Mchezaji Sergio Ramos anayelengwa na Manchester United msimu huu hataondoka Real Madrid kulingana na mkufunzi Rafael Benitez.
Ombi
la United la kutaka kumsajili beki huyo kwa kitita cha pauni milioni 28
lilikataliwa na Real Madrid ambayo inamwinda kipa wa Manchester United
David De Gea.
Lakini Benitez alisema:''Ninamuona Sergio kama kiungo muhimu cha timu yetu. Ni mshindi na hicho ndicho tunachokitaka''.
Rais wa Real Madrid tayari amesema kuwa Ramos atasalia katika kilabu hiyo.
Mkufunzi
huyo wa zamani aliyeifunza Liverpool na Chelsea ambaye alisajiliwa na
Real Madrid mwezi Juni,aliongezea:''Nimeongea na Ramos kwa urefu msimu
huu kuhusu hatma yake''.
No comments:
Post a Comment