Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, May 14, 2012

Jalili: Magharibi ibadilishe misimamo yake isiyo na tija kuhusiana na Iran

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameyatahadharisha madola ya magharibi kuhusiana na misimamo yao isiyo na tija kuhusiana na Iran.
Akizungumza hapa mjini Tehran na Michel Rocard Waziri Mkuu wa zamani wa Ufaransa, Saeed Jalili ameashiria utendaji wa kimantiki wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kutatua hitilafu kati yake na Wamagharibi na kuwatahadharisha viongozi wa madola ya Magharibi akiwataka wajiweke mbali na matamshi yasiyo na tija kuhusiana na Iran.
Jalili ameongeza kuwa, kutumia wenzo wowote ule wa mashinikizo dhidi ya Iran hakutokuwa na natija yoyote ya maana. Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema, kama kweli kundi la 5+1 linataka kufikiwe maafikiano baina yake na Tehran katika mazungumzo yajayo huko Baghdad, basi linapaswa kuonyesha nia njema.

No comments: