Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, April 28, 2012

Baadhi ya nchi zinafurahishwa na vitendo vya kigaidi nchini Syria

Naibu wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, nchi ambazo zinayatumia silaha magenge ya kigaidi nchini Syria, ndizo zinabeba dhima ya mauaji yanayoendelea nchini humo. Amir Abdullahian Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya nchi za Kiarabu na Kiafrika amesema kuwa, hivi sasa Syria imevuka hali ya ukosefu wa amani na kuelekea taratibu kwenye utulivu lakini baadhi ya nchi bado zinaendelea kuyatumia silaha magenge ya kigaidi kwa ajili ya kushadidisha mauaji katika nchi hiyo ya Kiarabu. Akilaani vikali vitendo vya kigaidi ambavyo vimepelekea kuuawa na kujeruhiwa wananchi wasio na hatia wa Syria Abdullahian amesema, mabadiliko yaliyofanywa na Rais Bashar al Asad wa Syria ni fursa nzuri kwa wananchi wa nchi hiyo. Aidha amewaunga mkono wananchi wa Syria na kuongeza kuwa, pamoja na kuwepo njama mbali mbali kutoka kwa nchi chache, Damascus itavuka vizingiti hivyo na kufikia hali nzuri na pevu.

No comments: