Wakuu wa jimbo la New South Wales la nchini Australia wana mpango wa kutumia mfumo wa kifedha wa Kiislamu katika jimbo lao.
Afisa mmoja wa serikali ya Australia amesema kuwa, ujumbe wa wataalamu wa huduma za taifa ukiongozwa na Barry O'Farrell, gavana wa mkoa wa New South Wales, wataelekea mjini Dubai Imarati Jumanne wiki hii kwa ajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Shirika la Maendeleo ya Usafirishaji Nje Bidhaa la Dubai kuhusu masuala ya kisheria na usimamiaji, ya mfumo wa fedha wa Kiislamu.
Naye Bw. Talal Yasin, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Crescent Wealth, ambalo ni la kwanza la Kiislamu nchini Australia na ambalo lina makao yake mjini Sydney amesema kuwa mfumo wa kifedha wa Kiislamu unazidi kupata nguvu katika jamii ya wafanyabiashara nchini Australia.
No comments:
Post a Comment