Mtawala wa Qatar, Sheikh Hamad bin Khalifa Aal Thani ameondoka
rasmi madarakani na kumuachua mamlaka manawe Sheikh Tamim bin Hamad Aal
Thani.
Amiri huyo mwenye umri wa miaka 61, ambaye aliingia madarakani mwaka
1995 baada ya kumpindua baba yake, sasa amemuachia madaraka mwanawe
mwenye umri wa miaka 33 katika hafla iliyofanyika kwenye mji mkuu wa
nchi hiyo, Doha.
Akizungumza kwa njia ya televisheni Sheikh Hamad bin Khalifa Aal
Thani alidai kwamba, uamuzi wake huo unalenga kuachia kizazi cha vijana
fursa ya kuongoza.
Duru zinaarifu kuwa, baraza la mawaziri pia litabadilishwa ili vijana
wachukue nyadhifa muhimu. Weledi wa mambo wanasema, mtawala huyo wa
Qatar amejiuzulu kufuatia mashinikizo ya Marekani.
Mfalme mpya wa Qatar, sawa na baba yake, anatazamiwa kuendelea kuwa kibaraka wa Marekani katika eneo hili la Mashariki ya Kati.
Itibari ya Qatar imeharibika kimataifa hasa kati ya Waislamu kutokana
na kujihusisha nchi hiyo ndogo na uungaji mkono kwa magaidi wanaotaka
kuiangusha serikali halali ya nchini Syria, na wakati huo huo kufanya
urafiki wa wazi na utawala wa Kizayuni wa Israel.
No comments:
Post a Comment