Tume ya uchaguzi ya Malawi imewahakikishia raia wa nchi hiyo pamoja na
jamii ya kimataifa kwamba uchaguzi mkuu wa Mei 20 utakuwa huru na wa
haki. Mwenyekiti wa tume hiyo, Maxon Mbendera amekanusha baadhi ya madai
ya wapinzani kwamba tume hiyo huenda ikashirikiana na chama tawala
kufanya uchakachuaji huku akisisitiza kuwa, teknolojia za kisasa
zitatumika kwenye zoezi la upigaji kura ili kuondoa uwezekano wa
kufanyika udanganyifu.
Raia milioni 7.5 wamejiandikisha kupiga kura
katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika. Uchaguzi mkuu wa Mei 20 utatoa
fursa kwa wananchi wa Malawi kumchagua rais, wabunge na madiwani. Kiti
cha urais kimewavutia wagombea 12 akiwemo Rais Joyce Banda. Uchunguzi wa
maoni unaonyesha kuwa, umaarufu wa Rais Banda umepungua mno na huenda
akashikilia nafasi ya tatu. Kiongozi huyo amepuuzilia mbali uchunguzi
huo wa maoni akisema umefadhiliwa na wapinzani ili kuwatamausha wafuasi
wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment