Klabu ya Liverpool nchini Uingereza
imetoa kitita cha pauni milioni 32.5 kwa Aston Villa kwa lengo la
kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 24 alifunga mabao 12 katika mechi 12 katika
msimu wa mwaka 2014-2015 na kuisadia Villa kusalia katika ligi kuu ya
Uingereza.
Liverpool inamtaka mchezaji huyo baada ya kupokea
kitita cha pauni milioni 49 kutokana na mauzo ya mchezaji Raheem
Sterling aliyehamia Mancity.
Benteke bado amesalia na kandarasi ya miaka 2 katika klabu ya Villa.
Mshambuliaji
wa Uingereza Daniel Sturridge aliichezea timu hiyo mara 18 msimu
uliopita kutokana na msururu wa majeraha na atasalia nje hadi mwezi
Septemba akiuguza jeraha la kiuno.
No comments:
Post a Comment