Duka la westagate lililo mji mkuu
wa Kenya Nairobi linafungua milango yake hii leo kwa umma karibu miaka
miwili tangu lishambuliwe na wanamgambo wa al shabab.
Watu 67 waliuawa wakati wa makabiliano ya siku nne wakati wanamgambo hao walipowafyatulia risasi wateja.
Duka
hilo linafunguliwa wiki moja baada ya rais wa Marekani Barack Obama
kufanya ziara nchini kenya hatua inayoonekana kama ishara ya imani kwa
usalama wa nchini Kenya.
Al Shabab wameendesha mashambulizi
mengine mabaya nchini Kenya tangu litokee shambulizi la Westgate
likiwemo la chuo kikuu cha Garissa ambapo watu 150 waliuawa.
No comments:
Post a Comment