Mazungumzo kati ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA yameanza katika mji mkuu wa Austria, Vienna. Kikao hicho kinahudhuriwa na timu ya mazungumzo ya Tehran ikiongozwa na Ali Asghar Sultaniye Mwakilishi wa kudumu wa Iran katika wakala huo, Herman Nackaerts Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Rafael Grossi Msaidizi wa Katibu Mkuu wa IAEA katika masuala ya kisiasa pamoja na wataalamu kadhaa wa wakala huo.
Nackaerts amewaambia waandishi habari kabla ya kuanza mazungumzo hayo kuwa, lengo la kikao hicho ni kufikiwa maafikiano kwa ajili ya kujibu masuala yote ambayo bado hayajatatuliwa kuhusu mipango ya nyuklia ya Iran hasa kuhusu madai yasiyo na msingi kwamba, kuna uwezekano mipango hiyo ikawa ya kijeshi.

No comments:
Post a Comment