Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran amesema leo kuwa,
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitafumbia macho haki zake za nyuklia
kwenye mazungumzo yanayoendelea kati yake na kundi la 5+1. Akiwahutubia
Waislamu kwenye hotuba ya pili ya Sala ya Ijumaa hapa Tehran, Hujjatul
Islam Kazem Siddiqi amesema timu ya mazungumzo ya Iran inajua vyema
mstari mwekundu uko wapi kwenye mazungumzo hayo na kwamba Wamagharibi
hawana haki ya kuitwisha Iran matakwa na mitazamo yao.
Sheikh Kazem
Siddiqi amesema, makubaliano ya mwisho kati ya Iran na Wamagharibi
sharti yatambue rasmi haki ya Iran ya kurutubisha urani ndani ya nchi
pamoja na kustafidi na teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani.
Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa Tehran pia amezungumzia masuala
mengine ya kieneo na kimataifa kwenye hotuba yake hiyo lakini kubwa
zaidi ni kuhusu suala la kujiimarisha kijeshi taifa la Iran kwa lengo la
kujiweka tayari kujibu hujuma zozote za maadui. Kuhusiana na hilo
Hujatul Islam Siddiqi amesema nia ya Iran ya kujiimarisha kijeshi si
kuzitisha nchi majirani bali lengo lake kuu ni kuhakikisha taifa liko
tayari wakati wote kukabiliana na hujuma zozote za maadui.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment