Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema kuwa, nchi yake
imefanikiwa kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka
mitano lakini akakiri kwamba idadi ya vifo vya akina mama wajawazito
bado iko juu. Rais Kikwete amesema Tanzania inaweza kufikia malengo
mengi ya milenia kufikia mwaka ujao wa 2015 iwapo sekta zote za serikali
na zile za kibinafsi zitashirikiana. Kiongozi huyo amesema Tanzania
imepiga hatua kubwa katika sekta ya afya lakini akasisitiza kuwa, bado
kuna kibarua cha ziada kinachopaswa kufanywa ili kuimarisha zaidi utoaji
huduma katika sekta hiyo.
Umoja wa Mataifa ulianzisha mpango wa Malengo ya Milenia mwaka 2000
ambapo nchi zote za dunia zilikubali kuweka mikakati ya kufikia malengo 8
ya milenia ifikapo mwaka 2015. Miongoni mwa malengo hayo ni kupunguzwa
umasikini kwa asilimia 50 katika kila nchi, kupunguzwa kabisa maambukizi
ya ugonjwa wa Ukimwi pamoja na kupanuliwa sekta za afya na elimu ili
watu wengi zaidi waweze kwenda shule pamoja na kupata huduma bora za
afya kote duniani.
No comments:
Post a Comment