Ofisi ya Takwimu za Taifa nchini Uingereza (ONS) imetoa ripoti
inayoonyesha kuwa, pengo kati ya tabaka la watu matajiri na lile la watu
masikini linazidi kupanuka kwa kasi. ONS imesema hali hiyo inatia
wasiwasi kwani mlingano katika jamii unazidi kupotea. Kwa mujibu wa
ripoti hiyo, matajiri wanazidi kuwa matajiri na masikini wanazidi kuzama
kwenye lindi la uchochole.
Wataalamu wa masuala ya uchumi wanasema hali
kama hiyo inaweza kusababisha ukosefu wa hali ya usalama na chuki za
kitabaka. Pia uchumi unaweza kuathiriwa na hali kama hiyo haswa
inapojitokeza kwamba masikini ni wengi kuliko matajiri.
Nchi nyingi za Magharibi ambazo zimeshindwa kudhibiti mlingano wa
kitabaka kati ya matajiri na masikini zinakabiliwa na matatizo mengi
hususan suala la usalama kama vile kuongezeka vitendo vya ujambazi na
mauaji ya kiholela. Marekani ni miongoni mwa nchi zinazosumbuliwa mno na
tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment