Baraza la Taifa la Mpito nchini Libya NTC limekanusha ripoti zilizoenea katika vyombo vya habari kwamba serikali ya mpito ya nchi hiyo imevunjwa. Mwenyekiti wa baraza hilo Mustafa Abdul Jalil amesema hakuna uamuzi kama huo uliochukuliwa. Siku ya Alhamisi, afisa mmoja wa ngazi za juu wa serikali ya Libya alisema kuwa NTC imeamua kumtimua Waziri Mkuu wa serikali ya mpito Bw. Abdur-Rahman Al-Keib pamoja na mawaziri wengine wa serikali hiyo lakini kwamba uamuzi huo ulikuwa haujatangaza rasmi. Weledi wa mambo wanasema kuwa migongano hiyo ya kauli inaashiria ukubwa wa nyufa zilizoko ndani ya NTC miezi 8 tangu ilipochukua uongozi wa Libya baada ya kuangushwa utawala wa kiimla wa Muamar Gaddafi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment