Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, April 29, 2012

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar si halali - Profesa Abdusharif + Sauti

Mwanahistoria mashuhuri wa visiwani Zanzibar amesema kuwa, muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauna uhalali wa kisheria, kikatiba na hata ridhaa ya wananchi.
Profesha Abdusharif amesema hayo katika mahojiano maalumu aliyofanyiwa na Radio Tehran na kutaja baadhi ya mambo yanayoondoa uhalali wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuwa ni pamoja na kutoshirikishwa wananchi na mabunge ya nchi hizo mbili katika uundaji wa muungano huo.
Vile vile amesema, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekuwa likichukua maamuzi ya upande mmoja bila ya kulishirikisha Baraza la Wawakilishi Zanzibar, jambo ambalo limezidi kupunguza mamlaka ya Zanzibar kadiri siku zinavyosonga mbele.
Aidha ametaka wananchi wapewa uhuru kamili wa kutoa maoni yao kwa uwazi na bila ya vitisho katika mchakato unaoendelea hivi sasa wa kutafuta Katiba mpya.
Bonyeza hapa kupata mahojiano hayo

No comments: