Kwa Mara nyingine tena Rais Barack Obama wa Marekani amedai kuwa ataweka
vikwazo vikali zaidi kwa Russia. Obama ametoa madai hayo kupitia
mazungumzo ya simu na Rais Francois Hollande wa Ufaransa kuhusiana na
kadhia ya Ukraine, ambapo sambamba na kuisifu serikali ya Kiev, Ukraine
kwa kuchukua hatua za lazima kwa ajili ya kuitisha uchaguzi wa rais wa
nchi hiyo inayokabiliwa na tishio la kugawika, amekariri tena vitisho
vyake dhidi ya Russia.
Aidha katika mazungumzo hayo ya simu kati ya
marais hao wa Marekani na Ufaransa wamejadili kuhusu kikao kilichopangwa
kufanyika mjini Paris kwa lengo la kujadili njia za kukabiliana na
kundi la Boko Haram la nchini Nigeria. Vitisho vya Obama dhidi ya
Russia, vimetolewa ikiwa ni siku moja tu ambapo John Kerry, Waziri wa
Mambo ya Nje wa Marekani ameitaka Russia kuiruhusu Ukraine kuendesha
uchaguzi wa rais katika tarehe iliyopangwa. Hata hivyo vitisho hivyo
vinaonekana havina taathira yoyote kwa serikali ya Rais Vladimir Putin
wa Russia na vinaonekana ni kama kelele za chura zisizoweza kumzuia
ng'ombe kunywa maji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment