Makumi ya maelfu ya waandamananaji wamejitokeza katika miji mingi ya
Uturuki na kupuuza wito wa Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan aliyewataka
wasitishe maandamano. Serikali imesema 'imedhibiti' maandamano katika
hali ambayo idadi kubwa zaidi ya waandamanaji ilikusanyika katika medani
ya Taksim mjini Istanbul ambayo ni kitovu cha maandamano ya kitaifa
ambayo yamekuwa yaliendelea uturuki kwa siku tisa sasa. Ghasia Uturuki
zilianza kufuatia mpango wa serikali wa kuharibu bustani ya Gezi karibu
na medani hiyo na badala yake kujenga maduka. Bustani ya Gezi imezoeleka
kuwa eneo la mijumuiko, mikusanyiko na maandamano na pia kivutio cha
watalii huku ikiwa ni sehemu pekee ya kijani ya umma iliyobakia kwenye
mji wa Istanbul.
Mamia ya watu wamejeruhiwa na wengine wengi kutiwa
mbaroni katika vurugu hizo. Waandamananaji aidha wamelaani vikali
msimamo wa Erdogan wa kuunga mkono magaidi wanaotaka kuiangusha serikali
ya wananchi wa Syria. Waturuki sasa wanataka Waziri Mkuu Erdogan
ajiuzulu na uchaguzi wa mapema kuitishwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment