Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema maafisa laki
mbili watasimamia uchaguzi kote nchini huku elfu sita kati yao wakiwa
katika vituo vya kupigia kura mjini Tehran.
Akizungumza na waandishi habari mjini Tehran, Waziri wa
Mambo ya Ndani Mostafa Mohammad-Najjar amesema wizara yake ina nafasi
muhimu katika kusimamia uchaguzi. Huku zikiwa zimebakia siku chache
kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na
vile vile wa mabaraza ya Kiislamu ya miji na vijiji, wizara ya mambo ya
ndani imebainisha sheria zitakazofuatwa katika uchaguzi. Najjar amesema
Wairani zaidi ya milioni 50 wametimiza masharti ya kupiga kura na kwamba
Wairani wanaoishi nje ya nchi pia watapata fursa ya kupiga kura katika
uchaguzi wa rais.
Uchaguzi wa rais wa awamu ya 11 utafanyika Juni 14 na
mshindi wa uchaguzi huo atachukua nafasi ya Rais Mahmoud Ahmadinejad
anayemaliza muda wake na ambaye kwa mujibu wa katiba hawezi kugombea
mara hii baada ya kuhudumu kwa mihula miwili mfululizo. Kuna wagombea
wanane wa kiti cha urais ambao ni pamoja Saeed Jalili, Ghulam Ali
Haddad Adel, Mohsen Rezai, Sheikh Hassan Rohani, Mohammad-Reza Aref,
Mohammad Gharazi, Mohammad Bager Qalibaf na Ali Akbar Velayati.
No comments:
Post a Comment