Watu 18 wameuawa katika mapigano makali baina ya makundi hasimu
ya wanamgambo wanaopigana kuudhibiti mji wa Kismayo kusini mwa Somalia.
Kwa mujibu wa wakaazi wa mji huo, watu 13 waliuawa jana Jumamosi na
wengine siku ya Ijumaa. Imearifiwa kuwa wanamgambo wa Ras Kamboni
wamechukua udhibiti wa eneo la Calanleey mjini Kismayo. Wanajeshi wa
Umoja wa Afrika kutoka Kenya ndio wanaosimamia usalama katika bandari
muhimu ya Kismayo na maeneo ya karibu. Oktoba mwaka 2012 wanajeshi wa
Kenya wakiungwa mkono na wanamgambo wa Ras Kamboni walichukua udhibiti
wa Kismayo kutoka kwa wapiganaji wa al-Shabab.
Afisa mwandamizi wa
al-Shabab mjini Kismayo Sheikh Xudayfa Abdirahman amedai kuwa Kenya ndio
iliyochochea mapignao ya hivi karibuni.
Baadhi ya wanasiasa wa serikali kuu ya Somalia wanadai kuwa Kenya
inataka kueneza satwa yake katika eneo la Jubaland ambalo mji wake mkuu
ni Kismayo. Hivi karibuni eneo hilo lilijitangazia mamlaka ya ndani na
kumteua Ahmed Mohamed Madoobe kama rais wake. Wakuu wa Mogadishu
wamebainisha upinzani wao kwa hatua hiyo.
No comments:
Post a Comment