Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, June 9, 2013

Kuakisiwa mdahalo wa tatu kwenye vyombo vya habari vya nje

Mdahalo wa tatu wa wagombea urais nchini Iran, umeakisiwa sana na vyombo mbalimbali vya nchi za nje. Shirika la Habari la Ufaransa, limeripoti kuwa, katika mdahalo mkali wa tatu na wa mwisho wa televisheni, wagombea wa urais katika uchaguzi wa wiki ijayo, wamekosoa siasa za baadhi ya wawakilishi wa mazungumzo ya nyuklia kati ya Tehran na madola yenye nguvu duniani. Shirika hilo la habari limeutaja mdahalo huo, kuwa uliojikita zaidi kuhusiana na siasa za mambo ya nje ya Iran huku maudhui kuu ikiwa ni kadhia ya nyuklia. Kwa upande wake Shirika la Habari la Associated Press limetangaza kuwa, wagombea wanane wa uchaguzi wa rais nchini Iran, walitofautiana kuhusiana na namna ya kuendesha mazungumzo ya nyuklia kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kundi la 5+1.
Nayo televisheni ya habari ya Bloomberg imetangaza kuwa, mdahalo wa siku ya Ijumaa kati ya wagombea urais nchini Iran, ulijikita katika masuala ambayo hayakutarajiwa kabisa.

No comments: