Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, June 9, 2013

Rais wa Senegal aonya kuhusu kuendelea mgogoro Magharibi mwa Afrika

Rais Macky Sall wa Senegal ameonya kuhusu  mgogoro katika nchi za eneo la Sahel barani Afrika bado haujamalizika. Sall amesema hayo katika mahojiano na gazeti la Kifaransa la Le Figaro linalochapishwa mjini Paris, na kuhusu hali ya kisiasa na kiusalama ya Mali ameeleza ana matumaini kuwa uchaguzi utafanyika mwishoni mwa mwezi wa Julai, kwa ushirikiano wa jamii ya kimataifa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS. Matamshi ya Macky Sall yametolewa huku mazungumzo kati ya wawakilishi wa serikali ya mpito ya Mali na kundi la kikabila la Tuareg juu ya upigaji kura katika mji wa Kidal yakianza leo Juni 8 katika mji mkuu wa Burkina Faso,Ouagadougou.
Hii ni katika hali ambayo, mapigano ya jeshi la nchi hiyo na Harakati ya Kitaifa ya Ukombozi wa Azawadi kaskazini mwa nchi, ni awamu mpya ya mgogoro huo ulioenea hadi  katika nchi nyingine za eneo la Sahel. Eneo la  Sahel la Afrika linazijumuisha nchi za Algeria, Chad, Senegal, Mauritania, Niger na Mali, ambazo zina makundi tofauti ya kabila la Tuareg yanayoishi kwa kuhama hama kwenye maeneo hayo. Maisha ya kuhamahama na ya kiasili ya Watuareg yamelifanya kabila hilo kuingia na kutoka kwa urahisi katika mipaka ya nchi za eneo hilo. Baadhi ya makundi ya kabila hilo yanajishughulisha na magendo ya madawa ya kulevya na binadamu pamoja na kuwatekaji nyara raia wa kigeni.
Mgogoro wa Mali ulioanza mwezi Machi mwaka uliopita baada ya mapinduzi ya kijeshi, yaliyoandaa mazingira ya kudhibitiwa eneo la kaskazini mwa nchi hiyo na Harakati ya Kitaifa ya Ukombozi wa Azawad na baadhi ya makundi yenye silaha yenye mfungamano na Watuareg. Kwa kutumia kisingizio hicho Rais Francois Hollande wa Ufaransa Januari 11 aliivamia kaskazini mwa Mali kwa madai ya kupambana na ugaidi. Kushindwa wanajeshi wa Ufaransa katika mapigano dhidi ya makundi ya upinzani yenye silaha kaskazini mwa Mali kuliilazimu Paris itangaza muda wa kuondoa askari wake magharibi mwa Afrika. Hata hivyo kubakia askari 1,000 wa Ufaransa kaskazini mwa Mali kwa kizingizio cha kushirikiana na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, kunadhihirisha jitihada za Paris za kuendelea kuweko kijeshi magharibi mwa Afrika. Vilevile kuruhusu askari wa Ufaransa harakati ya Azawadi  kwa mara nyingine idhibiti mji muhimu wa Kidal ni aina fulani ya uingiliaji wa Paris katika masuala ya ndani ya Mali. Ni wazi kuwa Ufaransa imeingilia masuala ya Mali kwa ajili ya kudhamini maslahi yake haramu katika eneo la Sahel. Vita nchini Mali ambayo vimepanuka hadi kwenye mipaka ya Niger, vimesababisha kusimama shughuli za shirika la kifaransa la Areva za kuzalishaji tani 350 za urani nchini Niger. Ufaransa inafanya jitihada ya kuendelea kudhiniti eneo la kaskazini mwa Mali kwa kutumia baadhi ya makundi kama vile harakati ya Azawadi , ili kulinda maslahi yake haramu kwenye eneo la Magharibi mwa Afrika.  

No comments: