Waziri wa Huduma za Anga za Misri Wael al Maadawi amesisitiza
kuwa, ndege zote za utawala wa Kizayuni wa Israel ambazo zitakuwa na
mfumo wa makombora, hazitaruhusiwa kutua kwenye viwanja vya ndege au
kupita kwenye anga ya nchi hiyo.
Al Maadawi amesema kuwa, hatua hiyo imechukuliwa baada ya shirika la
ndege la utawala wa Kizayuni wa Israel kudai hivi karibuni kwamba
limeamua kuweka mfumo wa kujilinda na makombora kwenye ndege zake zote
za abiria ili kulinda maisha na usalama wa abiria katika kukabiliana na
mashambulio ya kigaidi.
No comments:
Post a Comment