Kamati ya pamoja ya uchunguzi wa mipaka ya pamoja ya Ethiopia na Kenya
imetangaza kuwa, hakuna mabadiliko yoyote katika mpaka wa pamoja wa nchi
mbili hizo. Ripoti ya kamati hiyo imetolewa baada ya kukamilisha kazi
ya upitiaji mipaka ya pamoja ya Kenya na Ethiopia na kusisitiza kwamba,
mipaka ya nchi mbili hizo iko vile vile kwa mujibu wa makubaliano ya
uchoraji mipaka yaliyofikiwa na nchi hizo mbili mwaka 1970.
Kamati ya
pamoja ya ufundi ya kuchungumza mipaka ya Ethiopia na Kenya iliyoanza
kazi yake Mei 21 mwaka huu inajumuisha wataalamu wa masuala ya
jiografia, wataalamu wa mipaka ya kimataifa pamoja na washauri wa Wizara
za Mashauri ya Kigeni wa nchi mbili hizo walikuwa na jukumu la kupitia
na kuchunguza mipaka hiyo na kuibadilisha endapo wangekuta kuna
mabadiliko yoyote yale katika mipaka hiyo ambayo yanakinzana na
makubaliano ya mipaka ya mwaka 1970 yaliyofikiwa kati ya nchi mbili
hizo. Kenya na Ethiopia zina mpaka wa pamoja wenye urefu wa kilomita
779.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment