Rais Francois Hollande wa Ufaransa ameahidi kupambana na vitendo
vya uadui na chuki dhidi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu nchini humo.
Akizungumza mbele ya mjumuiko mkubwa wa wawakilishi wa taasisi na asasi
za kiserikali na kiraia pambizoni mwa Paris, Rais Hollande amesisitiza
kuwa, vitendo vya chuki na ubaguzi hasa dhidi ya Waislamu vinapaswa
kukomeshwa.
Miongoni mwa vitendo vya chuki na uadui dhidi ya wafuasi wa dini ya
Kiislamu mwaka huu, ni mashambulizi kadhaa yaliyofanywa dhidi ya
wanawake waliovaa hijabu ya Kiislamu katika eneo la Val- d'Oise
kaskazini mwa Ufaransa.
Viongozi wa Muungano wa Taasisi za Kiislamu
nchini Ufaransa UOIF wamesema kwenye mkutano na waandishi wa habari
kwamba, chuki na uadui dhidi ya Waislamu limekuwa jambo la kawaida
nchini humo na wamewataka viongozi wa serikali ya Paris kuvunja kimya
chao na badala yake kukabiliana na vitendo hivyo viovu.
Nalo Baraza la Utamaduni la Waislamu nchini Ufaransa CFCM limetangaza
kuwa, zaidi ya Misikiti 10 imeshavunjiwa heshima tokea kuanza mwaka huu
wa 2013.
No comments:
Post a Comment