Wamisri waishio katika nchi za kigeni wamepiga kura katika uchaguzi wa rais ambapo imebainika wengi wamewapigia kura wagombea wenye misimamo ya Kiislamu.
Katika mahojiano na kanali ya al Alam, Adel Sharif wa Chama cha Amal cha Misri amesema kuwa ushindi wa Abdel Moneim Aboul Fotouh katika duru hii ya uchaguzi ni ishara kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki. Aboul Fotouh ni mwanachama wa zamani wa Ikwanul Muslimin.
Ameongeza kuwa vyombo vya habari na wagombea wanaoupinga Uislamu wameshindwa katika njama zao za kuwaharibia jina wagombea wenye mielekeo ya Kiislamu. Adel Sharif amesema pamoja na kuwa wanasiasa wanaotaka Uislamu Misri hawana uwezo mkubwa katika uga wa vyombo vya habari, lakini wamepata mafanikio makubwa hadi sasa. Uchaguzi wa kwanza wa rais nchini Misri tangu dikteta Hosni Mubarak ang'olewe madarakani unatazamiwa kufanyika Mei 23 na 24.

No comments:
Post a Comment