Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, June 18, 2013

Malengo ya Rais Morsi wa Misri yafichuliwa

Mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati amesema kuwa lengo la Rais Muhammad Morsi la kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Syria lilikuwa ni kupata uungaji mkono wa makundi ya Kisalafi dhidi ya makundi yanayompinga nchini humo pamoja na kupata misaada ya kifedha kutoka Baraza la Mashirikiano la Ghuba ya Uajemi. Feisal Abdul Satir amesema kuwa, matamshi ya Rais Morsi dhidi ya Hizbullah na Syria yanaonyesha kuwa, kiongozi huyo wa Misri ameshindwa kusoma alama za nyakati kwani hivi sasa Uturuki inavuna chuki iliyoipanda nchini Syria.
Mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati amesema kuwa, Morsi ametumia kisingizio cha kuonyesha misimamo dhidi ya Hizbullah na Syria, kwa lengo la kupata misaada ya kifedha kutoka nchi za eneo la  Ghuba ya Uajemi.  Inafaa kuashiria hapa kuwa, mara baada ya makundi ya Kisalafi yenye kukufurisha watu wengine kutoa fatwa kuhusiana na Syria, Rais Morsi naye akachukua msimamo wa kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Syria.

1 comment:

Anonymous said...

Huyo si kiongozi anayestahili kuwaongoza raia wa Misri.... hana uzalendo kabisa na nchi yake