Rais Jakaya Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameonya kuwa mtu au kundi lolote litakalochachawiza mchakato wa kukusanya maoni ya Watanzania kwa ajili ya kuundwa katiba mpya atakiona cha moto. Aidha, amesema tume mpya ya katiba yenye wajumbe 30 inayotarajiwa kuanza kazi Mei Mosi, itahakikisha kuwa inazingatia maoni ya kila Mtanzania ingawa ametahadharisha kuwa maoni ya kuvunja Muungano hayatapewa umuhimu wowote. Rais Kikwete ametoa changamoto kwa Watanzania kutoa maoni yao kuhusu masuala mengine kama vile suala la mgombea binafsi, waziri kuwa mbunge na namna rais anavyochaguliwa. Amesema watakaojaribu kutumia fursa hiyo kuwagawa Watanzania kwa misingi ya kikabila, kidini au hata katika misingi ya muungano atakabiliwa na mkono mrefu wa sheria. Tume mpya ya Katiba Tanzania iliteuliwa Aprili 6 na inaongozwa na Jaji mstaafu Joseph Warioba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment