Mustapha Barghouthi mmoja kati ya viongozi wa mapambano wa Palestina
amejeruhiwa katika shambulizi lililofanywa na askari wa Israel.
Barghouthi alijeruhiwa jana katika shambulizi lililofanywa na jeshi
la utawala wa Kizayauni dhidi ya maandamano ya Wapalestina huko katikati
ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwenye mji wa Beitin. Kiongozi
huyo wa muqawamah wa Palestina amesema, askari wa Israel pia
wamewajeruhi makumi ya Wapalestina wengine waliotoka katika miji ya
Jenin, al Khalil, Nablus, Ramallah na Tulkarem kwenye tukio hilo.
Barghouth amesema, matumizi ya mabavu dhidi ya maandamano ya amani
hayatawazuia Wapalestina kupinga ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa
Kizayuni katika ardhi zao.
Hatua ya Israel ya kuendelea kupanua ujenzi wa vitongoji vya walowezi
wa Kizayuni katika ardhi za Palestina inazozikalia kwa amabavu imekuwa
kikwazo kikuu cha kupatikana amani Mashariki ya Kati. Umoja wa Mataifa
na nchi nyingi duniani zinasema kwamba, vitongoji hivyo vya Israel si
halala kwa kwamba vinajengwa katika ardhi za Palestina zilizoporwa
katika vita vya mwaka 1967 na Mkataba wa Geneva unazuia kujenga katika
ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
No comments:
Post a Comment