Habari kutoka mjini Mombasa, Pwani ya Kenya zinasema kuwa,
mshukiwa mmoja wa ugaidi amepigwa risasi na kuuawa. Mshukiwa huyo
alipigwa risasi baada ya kukataa kujisalimisha kwa polisi. Polisi
wanasema wamefanikiwa kupata maguruneti na zaidi ya bunduki mbili zikiwa
na risasi 200 nyumbani kwa mshukiwa huyo.
Mkuu wa polisi mjini humo, Aggrey Adoli amesema kuwa, mshukiwa
alikuwa anapanga kufanya mashambulizi ya kigaidi mjini Mombasa na
Nairobi.
Tukio hilo linakuja wiki moja baada ya watu sita kuuawa katika
shambulizi la kigaidi lililofanya dhidi ya kanisa moja mjini Mombasa.
Polisi wamekuwa wakiwalaumu wapiganaji wa kundi la al-Shabaab kwa
kufanya mashambulizi kama haya mara kwa mara nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment