Jeshi la Misri limetoa wito wa kudumishwa umoja baada ya
kuondolewa madarakani serikali ya Muhammad Mursi na kuapishwa Adly
Mansour kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo. Taarifa iliyotolewa na jeshi
imetaka kuimarishwa mshikamano wa kitaifa, haki na uvumilivu na kuongeza
kuwa, hekima, utaifa wa kweli na kujenga maadili ya binadamu masuala
yanayosisitizwa na dini zote yanahitajia kujiepusha na hatua za kipekee
na kiholela dhidi ya mrengo au kundi lolote la kisiasa.
Jeshi la Misri
aidha limesema, watu wanaweza kutumia haki yao madam hawavuki mipaka,
kwani maandamano yasiyokuwa ya amani yanaweza kuhatarisha usalama na
amani ya nchi.
Wakati huo huo harakati ya Ikhwanul Muslim ya Misri imeitisha
maandamano ya kupinga hatua ya jeshi la nchi hiyo ya kumuuzulu rais
Muhammad Mursi leo baada ya swala ya Ijumaa. Hayo yanajiri huku duru za
kiusalama zikiarifu kuwa, kiongozi mkuu wa harakati ya Ikhwanul Muslim
ya Misri Mohammed Badie amekamatwa na kupelekwa mjini Cairo.
No comments:
Post a Comment