Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, May 14, 2012

Rais Bashar al Assad: Saudia na Jordan zinataka kupindua serikali ya Syria

Rais Bashar la Assad wa Syria
Rais Bashar la Assad wa Syria amesema kwamba kwa mujibu wa taarifa za kuaminika Saudi Arabia na Jordan zinajishughulisha kufanya njama dhidi ya serikali ya Damascus katika mipaka ya kusini mwa nchi hiyo.
Assad amesema hayo katika mazungumzo yake ya mwisho na Kofi Annan mpatanishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika kadhia ya Syria. Assad amesisitiza kuwa, iwapo Syaria itashambuliwa na vikosi vya kigeni jeshi la nchi hiyo halitowaonea huruma wavamizi na kunyamazia kimya suala hilo.
Katika upande mwingine magenge ya kigaidi yanayopigana dhidi ya serikali ya Syria yamewaua askari 23 wa serikali na kujeruhi makumi ya wengine katika mji wa kusini wa Rastan. Katika mji mkuu Damascus na mji wa Dar'aa pia maafisa kadhaa wa polisi wameuawa. Duru mpya ya machafuko inashuhudiwa nchini Syria licha ya kutangazwa usitishaji mapigano kwa mujibu wa mpango wa amani wa Annan.

No comments: