Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia IAEA
amesema kuwa, licha ya kuongezwa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran,
lakini miradi ya nyuklia ya Iran inayofanyika kwa amani inazidi
kuendelea na vikwazo hivyo havina athari yoyote kwa nchi hiyo. Yukiya
Amano amesema kuwa, wakala wa IAEA una azma ya kuendeleza duru nyingine
ya mazungumzo ya nyuklia na Iran, ingawa tarehe ya kufanyika mazungumzo
hayo haijaainishwa.
Matamshi ya Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa IAEA yanatolewa katika hali
ambayo, Dakta Hassan Ruhani Rais Mteule wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
aliwaambia waandishi wa habari hapo jana kuwa, serikali yake
itahakikisha kuwa kuna uwazi katika mipango hiyo ya nyuklia ili
kuuthibitisia ulimwengu kwamba Iran ya Kiislamu haina nia ya kuunda bomu
la atomiki, bali miradi hiyo inafanyika kwa malengo ya amani.
No comments:
Post a Comment