Sudan Kusini ambayo imevamia eneo la Sudan la Heglig huko Kordofan Kusini imesema kuwa, haitoondoa vikosi vyake katika eneo hilo la mafuta hadi Umoja wa Mataifa utakapoingilia kati na kupeleka vikosi visivyopendelea upande wowote kwenye eneo hilo. Hii ni katika hali ambayo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetaka kusitishwa mara moja mapigano kati ya Sudan Kusini na Sudan yanayodaiwa kusababishwa na ugomvi wa mpaka. Hata hivyo Sudan imeilaumu Sudan Kusini kwa kuvuruga amani ya Sudan huku uchokozi huo wa Sudan Kusini dhidi ya Sudan ukilaaniwa na taasisi mbalimbali za kimataifa. Jumuiya mbalimbali ukiwemo Umoja wa Afrika zimelaani uvamizi uliofanywa na Sudan Kusini katika eneo la Heglig huko Kordofan Kusini na zimeitaka Juba kuondoka katika eneo hilo la Sudan haraka iwezekanavyo. Hatua hiyo ya Sudan Kusini imepelekea Sudan ijiondoke katika mazungumzo ya pande mbili yaliyokuwa yakisimamiwa na AU kwa lengo la kutatua mivutano kati ya nchi hizo mbili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment