Mahakama ya Libya imetangaza kuwa kesi inayowakabili Seiful Islam
Gaddafi mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi na
Abdullah Sanusi Mkuu wa zamani wa shirika la Kiintelijinsia la nchi hiyo
itasikilizwa mwezi Agosti mwaka huu nchini humo. Serikali ya Libya
imekataa kuwakabidhi watuhumiwa hao wa mauaji ya wananchi wa nchi hiyo
wakati wa utawala wa Gaddafi kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC
iliyoko nchini Uholanzi.
Hatua ya Libya ya kutaka watuhumiwa hao
wahukumiwe nchini humo imezua mivutano mikubwa na mahakama ya ICC kwani
mahakama hiyo ya kimataifa inadai kwamba, mazingira yaliyopo hivi sasa
nchini Libya hayawezi kuendesha kesi za watuhumiwa hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment