Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, June 17, 2013

Mazungumzo ya Bamako na Watuareg yaendelea

Mazungumzo ya mwisho kuhusiana na makubaliano ya kufanyika uchaguzi wa rais kati ya serikali ya Mali na waasi wa Tuareg, yameendelea huko katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou. Mazungumzo hayo ya pande mbili, yalifanyika hapo jana huku ajenda kuu ikiwa ni kadhia ya kufanyika uchaguzi wa rais katika mji wa Kidal kaskazini mwa nchi hiyo, unaodhibitiwa na waasi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso Djibril Bassole ambaye nchi yake ndio mpatanishi katika mgogoro wa Mali, amewambia waandishi wa habari kuwa, serikali ya Ouagadougou imewakabidhi wawakilishi wa serikali ya Bamako na waasi wa Tuareg ramani ya mpango wa makubaliano ya mwisho kuhusiana na kadhia nzima ya kufanyika uchaguzi wa rais katika jimbo la Kidal, nchini Mali.
Mazungumzo hayo yaliyoanza tarehe 8 mwezi huu nchini Burkina Faso chini ya usimamizi wa Rais Blaise Compaore wa nchi hiyo, yanajadili kuingia askari wa Mali mjini Kidal kwa ajili ya kusimamia uchaguzi huo wa rais uliopangwa kufanyika tarehe 28 mwezi ujao wa Julai.

No comments: