James Stuart Hall mtangazaji wa zamani wa redio na televisheni ya
serikali ya Uingereza BBC amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miezi 15
jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwabaka wasichana wenye umri mdogo
nchini humo. Peter Wright Mwendesha Mashtaka wa Uingereza amesema kuwa,
James Stuart Hall mwenye umri wa miaka 83 amekiri kutenda jinai hizo
wakati alipokuwa akiendesha moja ya vipindi maarufu kwenye shirika la
BBC katika miongo ya 70 na 80.
Amesema kuwa, kwa vile alikuwa mtu
mashuhuri, Hall alitumia fursa hiyo ya kujulikana mbele ya jamii wa
Waingereza katika kuwarubuni wasichana hao.
Baada ya kutolewa tuhuma dhidi ya Hall, maafisa wa polisi nchini humo
walianza uchunguzi dhidi ya Jimmy Savile mwendesha vipindi mwingine
mashuhuri wa BBC. Inafaa kuashiria hapa kuwa, shirika la BBC
lililazimika kuwaomba radhi wahanga na wananchi wa Uingereza baada ya
kufichuliwa kashfa ya kimaadili iliyowakumba watangazaji wa shirika hilo
la serikali ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment