Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, January 25, 2013

Mazungumzo ya amani Congo yasimama, Kampala

Mazungumzo ya kusaka amani kwa ajili ya maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baina ya ujumbe wa waasi wa eneo hilo na serikali ya Kinshasa yamesimamishwa.
Habari ya kusimamishwa mazungumzo hayo yaliyokuwa yakifanyika Kampala nchini Uganda imetangazwa na ujumbe wa waasi wa kundi la M23.
Mjumbe wa kundi hilo amesema kuwa mazungumzo hayo yamesimamishwa baada ya kutokuwepo maendeleo ya aina yoyote. Ameongeza kuwa kikao cha mwisho baina ya pande hizo mbili kilifanyika tarehe 18 Januari.

Waasi wa Congo wanaituhumu serikali ya nchi hiyo kwamba imepuuza makubaliano ya amani ya mwaka 2009 na wanadhibiti miji kadhaa muhimu ya mashariki mwa nchi hiyo. Mwezi Novemba mwaka uliopita kundi hilo la waasi liliuteka mji wa kistratijia wa Goma kwa siku kadhaa na kulazimika kuondoka katika mji huo kutokana na mashinikizo ya kieneo na kimataifa.

1 comment:

Unknown said...

Kwa nchi ya Congo si rahisi kupata muafaka kwani waliopo madaraka si wazalendo wa nchi yao....