Wananchi wa Bahrain wamefanya maandamano na kusisitiza kuundwa kamati
zisizoegemea upande wowote ili kuchunguza mateso wanayofanyiwa wafungwa
wa kisiasa nchini humo. Wananchi wa Bahrain jana usiku walifanya
maandamano makubwa huko Manama mji mkuu wa nchi hiyo na kutaka
kuhukumiwa wale wote wanaohusika katika uwanja huo.
Katika maandamano
hayo, wananchi wa Bahrain walipiga nara wakisisitiza juu ya udharura wa
kuachiwa huru haraka iwezekanavyo wafungwa wote wa kisiasa na kukomeshwa
mateso dhidi yao katika jela za utawala wa Aal Khalifa. Naye Sheikh Ali
Suleiman Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kitaifa ya al Wifaq amesisitiza
mwishoni mwa maandamano hayo juu ya udharura wa kukomeshwa ukiukwaji wa
haki za binadamu huko Bahrain na kueleza kuwa matabaka yote ya wananchi
nchini yanataka kuundwa serikali ya kiraia. Hii ni kwa sababu
wamechoshwa na ubaguzi na ukandamizaji wa utawala wa kifalme wa Aal
Khalifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment