Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, January 25, 2013

UTAJIRI WA BINTI WA RAIS DOS SANTOS WA ANGOLA NI 'KUFURU'.

Afrika ina bilionea wake wa kwanza wa kike, Isabel dos Santos, binti wa Rais wa Angola Jose Eduardo dos Santos.
Mwanamke huyo mwenye miaka 40 alisomea uhandisi katika chuo cha King's, mjini London, kabla ya kufungua biashara yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 24 - mgahawa unaoitwa Miami Beach.
Alichakarika kwa muda mrefu baada ya hapo, kwa sasa yuko katika bodi za makampuni kadhaa nchini Angola na Ureno na anamiliki hisa nyingi kwenye mashirika tajiri ikiwamo benki na kampuni ya Televisheni ya kulipia.

Utajiri wake ni pamoja na asilimia 19.5 za hisa katika Banco BPI, moja ya benki kubwa ya biashara nchini Ureno zenye thamani inayokadiriwa kufikia Dola za Marekani milioni 465 na asilimia 25 ya hisa katika benki ya Banco BIC ya Angola zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 160.
Mwaka jana mwanamke huyo aliripotiwa kuongeza hisa zake kwenye kampuni kubwa ya Televisheni za kulipia nchini Ureno ya ZON Multimedia kutoka asilimia 4.9 hadi 28.8 zenye thamani ya takribani Dola za Marekani milioni 385.
Hisa zote zikijumuishwa na vitegauchumi vingine zinasukuma utajiri wake hadi kufikia zaidi ya Dola za Marekani bilioni 1.
Hatahivyo kwa mujibu wa vyanzo vya jarida ya biashara la Forbes vilivyoko ndani ya Angola vinasema anamiliki pia asilimia 25 za hisa kwenye kampuni ya Unitel - moja kati ya kampuni mbili za mitandao ya simu nchini humo ambayo kwa mujibu wa wachambuzi ina thamani isiyopungua bilioni peke yake.
Angola, nchi yenye watu milioni 18, iko kwenye pwani ya magharibi ya kusini mwa Afrika na ina utajiri wa almasi na mafuta.
Jose Eduardo dos Santos amekuwa rais wa nchi hiyo tangu mwaka 1979, miaka minne baada ya kupata uhuru wake kutoka kwa Ureno.
Hivi karibuni alibadilisha katiba ya nchi hiyo na kujipatia miaka mingine kumi ya kutawala endapo chama chake cha MPLA kitashinda katika chaguzi zinazokuja.
Nchi hiyo iliandamwa na miaka 27 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo hatimaye vilikoma mwaka 2002 na kufuatiwa na ongezeko kubwa la mapato ya mafuta kutoka Dola za Marekani bilioni 3 mwaka 2002 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 66 mwaka 2008.
Transparency International, Shirika lisilo la Kiserikali linaloheshimika ambalo linachunguza ubadhirifu serikalini, hivi karibuni liliiweka Angola katika nafasi ya 168 kati ya nchi 178 katika orodha ya mtazamo wake kuhusu rushwa.
Katika jitihada zake za kufahamu kuibuka huko kwa ghafla kwa dos Santos, Forbes lilimuuliza Peter Lewis, Profesa wa Masuala ya Afrika katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins School for Advanced International Studies kuangazia mwanga katika masuala ya kibiashara nchini Angola.
Alisema: "Chanzo cha fedha na uongozi wa mashirika umekuwa wa utusitusi mno. Tatizo kuu katika Angola ni kukosekana kabisa kwa uwazi. Hatuwezi kuhisi chimbuko la fedha hizi.
Msemaji wa Isabel dos Santos nchini Ureno alisisitiza vitegauchumi vyake vyote vimewekewa uwazi wa kutosha kutoka katika orodha ya makampuni yaliyoorodheshwa hadharani.

No comments: