Vikosi vya Usalama Iraq vimewatia mbaroni magaidi 250 wenye
itikadi ya pote la Kiwahhabi na ambao wanapata himaya ya utawala wa
Saudi Arabia.
Magaidi hao waliokamatwa katika eneo la Euphrates ya Kati walikuwa
wakipanga njama ya kutekeleza oparesheni katika miji ya Iraq ya Karbala,
Najaf na ad-Diwaniya.
Kwa mujibu maafisa wa usalama wa Iraq, mkuu wa shirika la ujasusi la
Saudia Bandar bin Sultan ametoa dola milioni 250 kwa ajili ya kufadhili
oparesheni za kigaidi kote Iraq.
Aidha duru za usalama za Iraq zinasema Bandar bin Sultan amemkabidhi
makamu wa rais mtoro wa Iraq Tariq al Hashemi jukumu la kutekeleza
oparesheni za kigaidi nchini humo. Magaidi waliokamatwa wamekiri
kutekeleza mauaji ya malaki ya Wairaqi wasio na hatia.
No comments:
Post a Comment