Afrika Kusini imetangaza kuwa majeshi ya kigeni yanayopelekwa
nchini Mali kwa ajili ya kupambana na makundi ya waasi wa kaskazini mwa
nchi hiyo yanapaswa kuongozwa na nchi za Kiafrika.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Ibrahim Ibrahim amesema
kuwa operesheni ya majeshi ya kimataifa huko Mali inapaswa kuongozwa na
Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika (ECOWAS).
Majeshi ya Ufaransa yalianza mashambulizi makali huko kaskazini mwa
Mali Januari 11. Ufaransa ilichukua hatua hiyo kabla ya majeshi ya nchi
za Kiafrika kuwasili Mali kwa ajili ya kushiriki mwenye operesheni ya
kuwasaka waasi wa kaskazini mwa nchi hiyo wanaodhibiti miji kadhaa
muhimu ya eneo hilo.
No comments:
Post a Comment