Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, September 17, 2012

Obama kushitakiwa kuhusu kukejeliwa Mtume

Afisa wa ngazi za juu wa Iran amesema kwamba Rais Barack Obama wa Marekani anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria kuhusiana na kutengenezwa filamu iliyo dhidi ya Uislamu na Mmarekani Myahudi. Javad Muhammadi Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Utamaduni wa Kiislamu amesema leo kuwa, mashtaka yanaweza kupelekwa katika mahakama za Marekani dhidi ya Obama kwa kuvunja kipengele nambari 18 na 27 cha Makubaliano ya Kimataifa ya Haki za Kiraia na Kisiasa yanayohusiana na kuheshimiwa dini na imani za watu. Wakati huo huo mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Jihadul Islami ya Palestina amesema mwamko wa Waislamu katika kumtetea Mtume Mtukufu SAW ni kengele ya tahadhari kwa Wazayuni. Nafidh Azam ameongeza kuwa, wimbi la mwamko wa watu wenye hasira la kupinga kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad SAW ni kengele ya tahadhari kwa jinai za Wazayuni dhidi ya Msikiti wa al Aqswa.

No comments: