Balozi wa zamani wa Afrika Kusini huko Tel Aviv amesema Israel ni utawala wa kibaguzi.
Ismail Coovadia Balozi wa Zamani wa Afrika Kusini mjini Tel Aviv
katika barua aliyoawaandikia wanaharakati wa Palestina amesema, utawala
wa Israel ni sawa na utawala wa ubaguzi wa rangi uliokuwa madarakani
Afrika Kusini. Amesema kuwa mwaka 2012 alipomaliza shughuli zake Tel
Aviv, wizara ya mambo ya nje ya Israel ilimtaka apande mti katika
bustani ya wanadiplomasia lakini alikataa ombi hilo.
Ameongeza kuwa
hangeruhusu mti upandwe kwa jina lake au jina la Afrika kusini katika
ardhi ya Wapalestina iliyoporwa na Israel. Mwanadiplomasia huyo amesema
sera za Israel za kuwabagua Wapalestina ni sawa na yale yaliyoshuhudiwa
wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
Uhusiano wa Israel na Afrika Kusini umezorota katika miaka ya hivi
karibuni na kufika kiwango cha chini kabisa mwaka 2012 wakati Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Ebrahim Ismail Ebrahim
alipowataka watu wa Afrika Kusini kutotembelea Israel. Alisema Israel
inawadhulumu Wapalestina sambamba na kukalia ardhi zao kwa mabavu.
No comments:
Post a Comment