Rwanda imelituhumu jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na vikosi
vya Umoja wa Mataifa kwamba, vimeshambulia kwa mabomu vijiji kadhaa vya
Rwanda. Taarifa ya Rwanda imesema kuwa, jeshi la Congo na kikosi cha
askari wa kofia ya bluu wa Umoja wa Mataifa wamevishambulia kwa mabomu
vijiji viwili vya Rwanda jirani na maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
Kanali Joseph Nzabamwita msemaji wa jeshi la
Rwanda amewaambia waandishi wa habari kwamba, vijiji vilivyoshambuliwa
ni vya Kagashi na Gasiza vilivyoko kilomita takribani kumi na mbili
kaskazini mwa Rubavu. Ameongeza kuwa, maeneo yaliyoshambuliwa yako chini
ya udhibiti wa vikosi vya Congo DRC na vile vya Umoja wa Mataifa.
Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kila moja imekuwa ikimtuhumu
mwenzake kwamba, anayaunga mkono makundi ya waasi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment