Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, June 16, 2012

Duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Misri kuanza leo, Mohammed Morsi ana nafasi kubwa ya kushinda


Wananchi wa Misri leo wataelekea katika vituo vya kupigia kura kushiriki katika duru ya pili ya uchaguzi wa kumchagua rais mpya wa nchi hiyo baada ya wananchi kuuangusha utawala wa kidikteta wa Hosni Mubaraka. Katika uchaguzi huo Muhammad Mosri, mgombea wa harakati ya Ikhwanul Muslimin na ambaye ana nafasi kubwa ya kushinda, atapambana na Ahmad Shafiq aliyekuwa Waziri Mkuu wa mwisho wa utawala wa dikteta Mubarak.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri ametangaza kwamba usalama umeimarishwa nchini humo ambapo kumeongezwa idadi ya askari kwa ajili ya kulinda usalama katika vituo vya kupigia kura pamoja na ofisi za kampeni za uchaguzi na hali hiyo itaendelea hadi matokeo yatakapotangazwa. Uchaguzi huo utafanyika leo na kesho katika maeneo yote ya Misri.
Mwishoni mwa kampeni zake za uchaguzi Morsi amesema kwamba iwapo kura zitaibiwa basi kutatokea mapinduzi mengine makubwa nchini Misri dhidi ya watenda jinai ambayo yataendelea hadi pale malengo ya mapinduzi ya Januari 25 yatakapofikiwa.

No comments: