skip to main |
skip to sidebar
Iran yawatia mbaroni waliohusika na mauaji ya wanasayansi wake wa nyuklia
Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran imesema kuwa vyombo vya usalama vimewatia nguvuni watu waliohusika na mauaji ya wanasayansi wa nyuklia hapa mjini Tehran mwaka huu na mwaka 2010. Taarifa ya Wizara hiyo imesema uchunguzi mkali uliofanywa na vitengo kadhaa vya usalama umepelekea kukamatwa watu hao ambao kwa sasa wanashikiliwa huku wakiendelea kusailiwa. Waliokamatwa wamekiri kuwa na mfungamano na utawala haramu wa Israel. Mostafa Ahmadi Roshan, mwanasayansi wa nyuklia wa hapa Iran aliuawa mwezi Januari mwaka huu baada ya bomu kutegwa kwenye gari lake. Novemba mwaka 2010 mtaalamu mwingine wa nyuklia hapa nchini, Prof. Majid Shahriari aliuawa baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.
No comments:
Post a Comment