Watu wasiopungua 15 wameuawa na wengine zaidi ya 24 kujeruhiwa vibaya
katika shambulio la bomu lililofanywa katika msikiti wa Washia na
katika seminari ya kidini katika mji wa Peshawar huko kaskazini
magharibi mwa Pakistan. Maafisa wa usalama wa Peshawar wameeleza kuwa
shambulizo hilo lilitekelezwa wakati waumini wa Kishia walipokuwa katika
sala ya Ijumaa. Duru za kitiba pia zimearifu kuwa idadi ya waliouawa
katika shambulio hilo inatazamiwa kuongezeka kwa kuzingatia kuwa hali ya
baadhi ya majeruhiwa ni mbaya sana.
Hadi hivi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na mlipuko
huo wa bomu. Mlipuko wa leo katika msikiti wa Washia huko Peshawar ni
mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika mji huo tangu serikali mpya ya
Pakistan iingie madarakani mwezi Mei mwaka huu.
No comments:
Post a Comment