Wakati jua na mbingu za rangi ya samawati zinapofunikwa na mawingu, ardhi bado huwa na mwanga ambao hunufaisha mimea na viumbe wengine. Uislamu pia, sawa na jua, huleta uhai na nishati. Katika wakati ambao kumekithiri upotofu wa kinadharia na kiitikadi sambamba na njama za kuutenga Uislamu kupitia propaganda chafu, bado tunaona kuwa pamoja na kuwepo wingu la chuki za maadui, Uislamu ungali unaendelea kuleta uhai na nuru katika nyoyo za wapenda uhuru na watafutao haki. Kila siku tunaona nyoyo za watu wengi zikiukumbatia Uislamu. Hivi sasa mwangaza wa Qur'ani Tukufu unawavutia wanaadamu kwa njia isiyo na kifani na kwa hakika kitabu hiki kitukufu ndicho chanzo kikuu cha watu kuelekea katika Uislamu kwani Qur'ani ni muujiza wa kudumu milele wa Mtume SAW.
Ujumbe wenye nguvu wa Qur'ani
Nafasi kubwa ya Qur'ani katika jamii ya mwanaadamu inatokana na ujumbe wake wenye nguvu ambao unaweza kutumiwa na wanaadamu wote. Qur'ani Tukufu inajumuisha nukta za pamoja ambazo zinakubaliwa na wafuasi wa dini za mbinguni kama vile uadilifu, amani ya dunia, ubinaadamu, maadili mema, kupinga dhulma na kupambana na upotofu. Nukta hizi zinaifanya Qur'ani Tukufu kuwa kitabu cha muongozo wa dunia nzima.
Qur'ani Tukufu inawaita wanaadamu kuelekea katika tauhidi na utakasifu, yaani kumuabudu Mungu mmoja pasina kuwepo na taasubi na ubinafsi. Mwenyezi Mungu katika aya ya 64 ya Sura Aal Imran Qur'ani Tukufu anasema:
"Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lililo sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu."
Leo pamoja na kuwepo propaganda kubwa katika nchi za Magharibi dhidi ya Uislamu na Waislamu, tunashuhudia kuongezeka kila leo idadi ya watu wanaofanya utafiti wa kina kuhusu Qur'ani na dini ya Uislamu.

Wasemavyo wasomi Wamagharibi kuhusu Qur'ani
Utafiti kuhusu Uislamu na Qur'ani katika nchi za Magharibi ulianza katika zama za Renaissance na ungali unaendelea hadi zama zetu za leo. Goethe, mwanafalsafa na malenga Mjerumani anasema hivi kuhusu adhama ya Qur'ani baada ya kuisoma: "Inamvutia mtu mara moja, inashangaza na hatimaye inatufanya tuinyenyekee. Muundo wake, kwa mujibu wa maudhui zake, ni imara, adhimu na daima itabakia kuwa na athari kubwa.'
Profesa Henry Corbin mwanafalsafa Mfaransa anasema kwa mtazamo wake kwamba, moja ya nukta muhimu katika Qur'ani Tukufu ni wito wake wa kuwataka wanaadamu waongeze elimu yao. Anaendelea kusema kuwa 'kama fikra za Mtume Mohammad SAW zilikuwa potofu na iwapo wahyi aliopokea haukuwa wa Mwenyezi Mungu basi hangethubutu kuwataka wanaadamu watafute elimu. Hakuna mtu yeyote, kwa njia yoyote na mbinu ya kifikra, aliyeweza kutoa wito kwa wanaadamu kutafuta elimu kwa kiasi alichofanya Mtume Muhammad SAW na Qur'ani. Katika Qur'ani Tukufu aya mbali mbali zimetaja elimu, fikra na akili mara 950.'

Muaustralia aliyesilimu asema: 'Mimi ninaye Allah SWT'
Bi. Zeinab Taylor ni mmoja kati ya watu waliosilimu baada ya kumtambua Allah SWT na kunyenyekea mbele ya adhama ya Uislamu. Hivi sasa maisha yake yamejaa nuru kutokana na kufuata mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu. Juni mwaka 2008 alifika katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa lengo la kushiriki katika kongamano la kimataifa kuhusu shakhsia ya Bibi Fatima Zahra AS ambapo alibainisha namna alivyosilimu kwa kusema:
'Mimi natoka Australia ambayo ni nchi inayotafautiana na Iran. Ninakotoka Waislamu ni wachache sana. Awali nilikuwa Mkristo hadi pale rafiki yangu, kupitia mapenzi ya Mwenyezi Mungu, aliponipa vitabu kuhusu Uislamu. Vitabu hivyo vilinivutia sana, tab'an kitabu kilichonivutia zaidi na ambacho ni muhimu zaidi ya vyote alivyonipa ni Qur'ani Tukufu. Niliisoma kwa kina Qur'ani kabla ya kusilimu. Hisia niliyopata katika kitabu hiki ilibainisha wazi kuwa si cha ardhini bali ni cha mbinguni. Qur'ani kwangu mimi ndio muongozo bora zaidi kwa ajli ya kufahamu Tauhidi na maadili mema. Mafundisho yake yanaenda sambamba na mahitaji ya mwanaadamu wa dunia ya leo na kwa hakika Qur'ani inaweza kufuatwa katika zama zote. Kwa mtazamo wangu, mwanaadamu angali anahitaji kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na muumba na mwenye kuleta uhai. Mimi daima nilikuwa na hisia ya hitajio hili. Ingawa nilikuwa naendeleza uhusino huu kupitia dua na maombi ndani ya moyo wangu, lakini uwezeshaji wa uhusiano huu kupitia maneno ya Mwenyezi Mungu mwenyewe ni jambo linaloleta utulivu. Awali niliisoma Qur'ani kwa Kiingereza kisha kwa Kiarabu. Baadaye nilijifunza kuhusu Seerah au maisha ya Mtume SAW. Niliujua Uislamu hatua kwa hatua."
Kuhusu hali yake ya hivi sasa, Bi. Taylor anasema hivi:
'Hivi sasa nina uhakika kumhusu Mwenyezi Mungu. Nina imani kamili. Iwapo kuna taa ya muongozo katika dunia, basi ni Uislamu.'
Waliosilimu kote duniani, baada ya kuuchagua Uislamu hukabiliwa na vizingiti na matatizo mengi. Lakini utamu wa kuuamini Uislamu huwapelekea waendelee na njia yao bila kuyumba.
Bi. Zainab Taylor amepata matatizo mengi akiwa Mwislamu nchini Australia. Anasema hivi: "Nilikuwa mwanamke wa kwanza kuvaa Hijabu katika eneo langu. Ninaweza kusema kuwa uhusiano wangu na familia pamoja na marafiki zangu ulizorota wakati nilipoikubali dini ya Kiislamu. Kwa kweli kusilimu katika mazingira hayo ni Jihadi. Aghalabu ya watu walishtuka kuona mavazi yangu ya Kiislamu. Wengi walijitenga nami. Lakini pamoja na masaibu haya yote, nukta iliyonituliza na kuwa tegemeo langu ni Uislamu na Qur'ani. Mimi nina uhusiano na ambaye wao hawana. Mimi ninaye Allah SWT."
Ingawa anakumbana na matatizo mengi, lakini ana moyo uliojaa matumaini na wenye kudhihirisha kina cha imani yake, anasema hivi: 'Pamoja na hayo niliyoyataja, nina furaha na nina bahati. Hii ni kwa sababu mume wangu na watoto wangu nao pia ni Waislamu.'

Bishara njema ya Qur'ani kwa walioamini
Hivi ndivyo Allah SWT anavyoeneza Uislamu kupitia nuru ya Qur'ani Tukufu. Katika aya ya 25 ya Sura al Baqara Mwenyezi Mungu SWT anasema:
Na wabashirie walioamini na wakatenda mema kwamba watapata mabustani yapitayo mito kati yake; kila watapopewa matunda humo, watasema: Haya ndiyo kama tuliyopewa mbele (zamani). Na wataletewa matunda yaliyofanana; na humo watakuwa na wake waliotakasika; na wao humo watadumu.

No comments:
Post a Comment