Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, June 16, 2012

Rais wa Ivory Coast azitaka nchi jirani kuimarisha usalama wa mipaka


Rais Alasaane Ouattara wa Ivory Coast ameashiria kuongeneza mashambulizi ya wanamgambo nchini mwake na kuzitaka nchi jirani za Siera Lione, Liberia na Guinea Bissau kushirikiana na nchi yake katika kuimarisha usalama kwenye maeneo ya mpakani. Aidha ameashiria kwamba kuungana nchi hizo ni jambo la dharura na kusema kwamba muungano huo unapaswa kuwa kati ya nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS.
Taarifa mbalimbali zimewanukuu viongozi wa Kodivaa wakisema kuwa, mashambulizi ya wanamgambo wenye silaha nchini humo yanaratibiwa katika ardhi ya Liberia.
Liberia ilifunga mpaka wake na Ivory Coast baada ya kushadidi mashambulizi hayo.

No comments: