Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, June 15, 2012

Mahakama ya Katiba ya Misri yaamua Shafiq anaweza kuendelea kugombea urais

Mahakama ya Katiba ya Misri imeamua kuwaAhmad Shafiq aliyekuwa Waziri Mkuu wa mwisho wa utawala wa Hosni Mubarak aliyepinduliwa nchini humo anaweza kugombea katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais itakayofanyika wikiendi hii. Mahakama hiyo ilikuwa imetakiwa kuamua juu ya sheria iliyopitishwa na bunge ya kuwapiga marufuku wale wote waliohudumu katika utawala wa Hosni Mubarak kugombea urais nchini humo.
Aidha ya Mahakama ya Katiba ya Misri imetoa hukumu kwamba theluthi ya wabunge walichaguliwa kinyume cha sheria za katiba ya nchi hiyo na kubatilisha ubunge wao, lakini bado haijajulikana iwapo viti vya wabunge hao vitagombewa tena au la.
Katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Misri itakayofanyika Juni 16 na 17 Shafiq atapambana na mgombea wa harakati ya Ikhwanul Muslimin Muhammad Mursi.

No comments: