Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, May 15, 2012

ICC yafungua mashtaka mapya dhidi ya Wakongo wanaosakwa

Jenerali Jean Bosco Ntaganda
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imefungua mashtaka mapya ya jinai za kivita dhidi ya wababe wawili wa kivita wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yaani Jenerali Jean Bosco Ntaganda na Sylvestre Mudacumura.
Shirika la Habari la Ufaransa limemnukuu Mwendesha Mashtaka Mkuu wa mahakama ya ICC, Luis Moreno-Ocampo akisema jana kuwa, Ntaganda na Mudacumura ni watu wawili hatari sana katika eneo ambalo mamilioni ya watu wameuawa katika mapigano ya miongo miwili iliyopita.

Jenerali Ntaganda ambaye ni mashuhuri kwa vitendo vyake vya ukatili, amekuwa akitafutwa na mahakama ya ICC tangu mwaka 2006 akikabiliwa na mashtaka mbalimbali ya jinai za kivita ikiwa ni pamoja na kuwalazimisha watoto wadogo kuwa wanajeshi.
Huku hayo yakiripotiwa, jana eneo la mashariki mwa Congo lilishuhudia mapigano makali kati ya waasi na jeshi la Congo. Waasi wengi wanaoongozwa na Jenerali Ntaganda, ni wanajeshi wa serikali walioasi.
Wakati huo huo askari 11 wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wamejeruhiwa na wanavijiji wenye hasira mashariki mwa Congo ambao wanalalamika kuwa, askari hao wa Umoja wa Mataifa wameshindwa kuwalinda.
Zaidi ya Wakongomani 10,000 wameripotiwa kukimbilia Rwanda na Uganda katika kipindi cha siku chache zilizopita.

No comments: